Home » » UPENDO

UPENDO

                                           UPENDO  NI  TUNDA LA MSAMAHA
                  SAYS MATANDA RICHARD   TESHA

UTARATIBU SAHIHI WA KUMSAMEHE/KUSAMEHEWA

1. Mtu aombe msamaha kwanza au atubu ndipo asamehewe?
2. Asamehewe hata pasipo kuomba msamaha?
3. AU Vyote viwili ni sawa ?


JIBU  :  VYOTE VIWILI NI SAWA.


KWANINI NIKUSAMEHE,
naamini umeshajifunza mengi sana juu ya          kusamehe na kusamehewa na leo nataka nikuongezee au nikupe namna nyingine ya kuona juu ya hili jambo.Kusamehe ni kutomuhesabia mtu hukumu kwa jambo ambalo amefanya kwa kukusudia au kutokukusudia.Ni kusahau na kuachilia.Na ninapenda sana kuelezea hili ili tujue nafasi ya kusamehe katika mafanikio yetu ya kila siku na mpaka ule uzima udumuo milele.Watu wengi wamekuwa si wepesi wa kusamehe pale wanapokosewa na watu na wengine ni wepesi sana wa kuwasamehe watu wanapowakosea.Utofauti uliopo kati ya hao watu ni utofauti kati ya kujua na kutokojua nguvu ya NEEMA ya Mungu maishani mwetu.Na leo nataka nielezee sababu tatu tu za kwanini tunatakiwa kusaheana


· Usimsamehe mtu kwa sababu ni adui au rafiki       
             yako,      
· Ni  jirani yako,
· Ni  amekukosea sana, amekukosea kidogo,
· Amekukosea  mara chache au mara mia,
· Ni  mrefu au mfupi,
· Ni  mwembamba,kabila lake,
                  Umri  wake.

Mama Bikira Maria anasamehe wote walioshiriki kuua mwanae wa pekee. Wewe je! Ukotayari kuwasamehe wote waliokuumiza katika maisha yako? Fanya hivyo ufungue milango ya Baraka.

1 comments:


  1. VITU VITATU AMBAVYO NI VIPIMO KAMA UMESAMEHE AU BADO HUJASAMEHE:


    1.       Ukimsamehe mtu utamwongelea vizuri:

    Kama kweli umemsamehe mtu utamwongelea vizuri mbele za watu, kama unasema umemsamehe mtu alafu bado unamwongelea vibaya ujue bado hujasamehe kutoka moyoni mwako. Ukimkuta mtu anaongea mabaya kuhusu mtu aliyemkwaza basi ujue ndani ya moyo wake kuna madabahu ya makwazo na machungu. Na kwasababu hiyo kuna watu wamefukuzwa kazi, wamepigwa kwasababu ya kushindwa kuwanenea watu mazuri.
     
    2.       Ukimsamehe mtu utamwombea:

    Ishara nyingine kuwa ya kuonyesha kuwa umesamehe ni kumwombea mwingine mazuri; na ndio maana Eliya alipotaka kujenga madhabahu ya Mungu alibomoa kwanza madhabahu ya baali, hata leo huwezi kujenga madhabahu ya Mungu ya amani kama bado moyoni unamadhabahu ya kutokusamehe. Watu wengi wamejikuta wakiomba mabaya kwa watu waliowakosea na kwa namna hiyo wanashindwa kupokea majibu ya matatizo yao.
     
    3.       Ukimsamehe mtu utawasiliana kwa uzuri:

    Ukimsamehe mtu utawasiliana naye kwa uzuri, nah ii ni kwenye madhabahu ya moyo wako. Hata kama amekujibu vibaya wewe mjibu kwa uzuri. Ni kweli kuwa ukisamehe Yule mtu atakudharau lakini ni muhimu kujua kuwa tunasamehe si kwa ajili ya waliotukosea bali kwa ajili yetu. 
    Watu wengi wanashindwa kusamehe kwasababu ya kukosa nguvu ya uwezesho ya kuweza kusamehe. Kila mtu aliyeokoka anayo nguvu ya uwezesho ya kusamehe, nayo ni Roho Mtakatifu. Kila mtu aliyeokoka ana Roho Mtakatifu naye hutuwezesha kusamehe, kuokoka kunakupa nguvu ya uwezesho kusamehe. Bila kusamehe huwezi kupokea kutoka kwa BWANA.

    ReplyDelete

RICHARD MATANDA TESHA

 
Support : Richie | Bikira Maria | Elimu Endelevu
Copyright © 2013. BIKIRA MARIA - All Rights Reserved
Template Created by Mwariko Published by Mwariko team
Proudly powered by Jicho la Habari