Home » » MARIA KAMA ZAWADI YA MUNGU KWETU

MARIA KAMA ZAWADI YA MUNGU KWETU





    MARIA KAMA ZAWADI YA MUNGU
MATANDA RICHARD TESHA 
 
Maria alipendelewa na Mungu kwasababu alimchagua kuwa mama wa mtoto wake ambae atakuwa mkombozi wa dunia nzima atakayemwokoa mwanadamu kutoka mitego ya shetani na dhambi.
Maandiko  matakatifu yanatuambia kuwa mama huyu amejaa neema na Mungu yuko pamoja naye (Lk 1:28) salamu hii ya malaika Gabriel inakuwa chanzo cha sala zetu ( salamu Maria umejaa neema Bwana yu nawe umebarikiwa kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa,maria mtakatifu mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu amina.) mpendwa nakualika kuisali sala hii kwa utulivu na kutafakari kila unachokisema. Tunaona hapa kwamba Mungu alipaanda mahali pa kuishi katika harakati za kuanza ulimwengu mpya uliokombolewa.
Wanateolijia na baba watakatifu ambao walihusika sana katika kuanda misingi imara juu ya mama yetu. Ukweli kwamba yeye alikingiwa dhambi ya asili anakuwa kiumbe cha juu sana kupita vyote vinavyozaliwa na dhambi ya asili. Mt. Thomas wa Akwino alisema kwamba kila kilicho kikamilifu kinapatikana katika nafsi ya B.Maria. na kila kitu ambacho watakatifu wanacho kama karama yao mama Bikira anacho kwa ukamilifu wake( mf. Kama mtakatifu Fulani alikuwa mpenda watu sana mama bikira maria anakipaji hicho kwa ukamilifu wake).
Mama  Bikira Maria ana ukaribu wa pekee na mwanae(Bwanawetu Yesu Kristu).Ikiwa na maana kuwa alishirikiana na anashirikiana na mwanae katika kazi ya kumkomboa mwanadamu. Alishirikiana naye kwa kila hali katika harakati za kumkomboa mwanadamu. Mama huyu anasimama kinyume na Eva mwanamke wa kwanza na mama wa wote wenye mwili. Kila kilichopotea kwa ajili ya Eva kimerudishiwa hadhi yake na B.Maria. mt. Augustino alithibitisha ukweli huu aliposema “Hapa tunagundua fumbo kubwa;kwamba katika mwanamke tunakufa na katika mwanamke tunarudishiwa uzima”. Na kwa hali hiyo kutokana na imani yetu ya kikatoliki tunapata kujua kuwa kufanyika mtu kwa mwana wa Mungu au kuja kwa mkombozi kuna uhusiano na dhambi ya asili anguko la wazazi wetu wa kwanza(Adamu na Eva)

1 comments:

  1. mfanye mama huyu kuwa mwombezi wako. alifanya mengi katika harakati ya ukombozi wako. asiye sikia la mkuu huvunjika guu. says fr. matanda

    ReplyDelete

RICHARD MATANDA TESHA

 
Support : Richie | Bikira Maria | Elimu Endelevu
Copyright © 2013. BIKIRA MARIA - All Rights Reserved
Template Created by Mwariko Published by Mwariko team
Proudly powered by Jicho la Habari