Home » » BIKIRA MARIA MKINGIWA DHAMBI YA ASILI

BIKIRA MARIA MKINGIWA DHAMBI YA ASILI

Ili mwana wa Mungu kuwa mwanadamu na kutukomboa ,nafsi ya pili ya utatu mtakatifu alipaswa kuwa na mama wa kibinadamu ambaye ni B.Maria. sasa naomba tuangalie hatua ambazo Mungu alizichukua ili kumpata mama wa Mkombozi.
Lengo la mwokozi ni kumkomboa mwanadamu kutoka utumwa wa shetani na dhambi,na haingekuwa jambo jema mkombozi ahusike na dhambi kwa nanma yoyote. Ndiyo maana tunasema yeye alikuwa mwanadamu kama sisi isipokuwa hakuwa na dhambi. Kutokana na muono huo wa Mungu,alimkinga B.Maria na dhambi ya asili. Mpendwa bilashaka unajua kuwa kila mwaka tunasherekea sikukuu ya B.Maria Mkingiwa dhambi ya asili tarehe 8/12 kila mwaka; sina uhakika kama baadhi yetu leo hii tunatambua sherehe hii na maana yake. Kuna kipindi katika historia ya kanisa ambapo dalili za kuelewa sikukuu hii inajiodhihirisha lakini leo hii wapo wengi wasiotambua na ndio maana ifikapo sikukuu hii hata kwenda kanisani inakuwa shida sana. Tuaalikwa kujirudi na kutambua tunu zetu katika imani yetu.
Funzo imani hili juu Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili lilitangazwa na Baba mtakatifu Pius IX huko Roma tarehe 8/12/1854. Funzo hili  linamaanisha kuwa Bikira Maria alikingiwa na dhambi ya asili kuanzia pale alipotungwa mimba. Mama yetu mpendwa Bikira Maria allizaliwa kama wanadamu wengine wazazi wake wakiwa Anna na Joachim.
Mpendwa,ili kuelewa kanisa linamaanisha nini na fundisho hili,ni vizuri kukumbuka kuwa Neema ya utakaso kabla ya anguko lao. Hawa ndio wazazi wetu wa kwanza kabisa. Adamu hakuwa tu baba yetu alikuwa pia kioo cha maadili ya jamii ya wanadamu na Mungu alimjaribu, hapa namaanisha kuwa angerithisha kwa watoto wake neema aliyokuwa nayo kama angekuwa mtii kwa Mungu aliyemuumba. Hivyo kuwa na Neema hiyo ya kimungu au kukosa neema hiyo kulitegemea sana utii  na uaminifu wa Adamu baba yetu kwa Mungu baba yetu.
Msikilizaji mpendwa,sote tunaelewa kilichotokea. Adamu alitenda dhambi na akapoteza neema si kwake tu lakini nasi sote tukaikosa kwa sababu yeye alituwakilisha sote. Ndiyo maana tunazaliwa tukiwa tuanakosa vitu ambavyo tungepaswa kuwa navyo kama neema ya Mungu. Mama kanisa anaita hali hii “ dhambi ya asili”. Lakini kwa neema yake Kristu aliturudishia neema tuliyoipoteza kwa maisha yake,mateso na kifo na kwa njia ya ubatizo tunarudishiwa mema ya kimungu na kuwa watoto wa Mungu na warithi wa mbinguni.
Dhambi ya asili inaelezeka kama kujitenga na Mungu na kuwa katika utumwa wa Yule mwovu. Kutokana na ukweli huu wababa wakanisa wanajiuliza hivi inawezekanakweli kuwa Bikira maria ilikuwa mtumwa wa shetani hata mara moja? Lahasha !Walivyotafakari kwa kina sana jambo hili walifikia hatua ya kusema Mama Bikira maria alikingiwa dhambi ya asili. Maandiko matakatifu yanaashiria jambo hili la kukingiwa dhambi ya asili ingawa si kwa uwazi kabisa. Mara tatu hivi wababa wanatumia maneno yafuatavyo kama kiashiria’ kitabu cha mwanzo sura 3:15 “nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke,kati ya uzao wako na uzao wake;yeye atakiponda kichwa chako nawe utamwuma kisigino chake.”,Luka 1:28-“malaika akamwendea,akamwambia,’salamu,ewe uliyeneemeshwa na Mungu!Bwana yuko nawe!”, na Luka 1:41 –“mara tu Elizabeth aliposikia sauti ya maria,mtoto mchanga tumboni mwake Elizabeth akaruka. Naye Elizabeth akajazwa Roho Mtakatifu. Mwanzo 3;15 inatafsiriwa kama uzao wa Eva (ie kristo Yesu) atamshinda Yule mwovu,lakini Yule mwovu pia atawatesa wafuasi wake kwa kuwashawishi kutenda dhambi
Hali hii mpendwa msikilizaji iliwapelekea wababa wakanisa kumwona mwanamke anayezungunziwa katika mwanzo 3;15 kama kivuli cha Bikira Maria mama wake Kristo. Wataalamu wengi wakisasa wa teolojia  wanasema kutokana na mwanga wa aya hii kuwa ushindi wa mama huyu dhidi ya Yule mwovu usingewezekana kama alikuwa na dhambi. Hivyo mama huyu aliingia duniani bila dhambi ya asili

1 comments:

RICHARD MATANDA TESHA

 
Support : Richie | Bikira Maria | Elimu Endelevu
Copyright © 2013. BIKIRA MARIA - All Rights Reserved
Template Created by Mwariko Published by Mwariko team
Proudly powered by Jicho la Habari