BIKIRA MARIA
MSAADA WA WATU. (ADIUTRICEM
POPULI – HELPER OF THE PEOPLE)
Tarehe 5/9/1895 baba
mtakatifu Leo XIII alitoa waraka wake wakichungaji kuhusu Rozari wenye kichwa
cha habari “ msaada wa watu”- Adiutricem Populi. Katika waraka wake huu
aliwaasa waamini kusali Rozari kwa mama yetu mpendwa aliye mama wa Kanisa.
Anatoa sababu ya kumwita Bikira Maria mlinzi wa wanakanisa. Maria alikuwa na
wajibu wa kuwafanya wanakanisa kuwa wamoja na kuimarisha imani ya kanisa.
Wakati Yesu alipopaa mbinguni mama alibaki hapa duniani kuongoza hatua za awali
kabisa za kanisa na kuwatia moyo mitume kwa kazi yao ya kuenezan Injili. Na
alipopalizwa mbinguni anaendelea na amefanya hivyo mara nyingi katika historia
ya kanisa alivyoingilia mambo mbalimbali ili kuamsha imani ya waamini na kuepuka
uzushi mwingi uliokuwa unaenea kila mahala.
Baba mtakatifu aliendelea
kussema watu waendelee kusali kwani kwa msaada wa mama, makanisa ya mashariki
yatarudi katika kundi moja. Katika mtaguso waw Efeso, wakristo wa mashariki na
magharibi walijumuika pamoja katika umoja mbele ya Bikira Maria katika ibada
moja. Ndio maana ibada ya mama yetu inatiliwa sana maanani kwani huleta watu
pamoja.
Baba huyu mtakatifu Leo XIII
aliwaalika wakristu wote kumwomba sana huyu mama Bikira Maria ili kuweza kuleta
pamoja watoto wake wote katika kanisa moja. Ndiyo maana mpendwa mwanafamilia
tunaposali litania ya Bikira Maria tunasali (Auxilium christianorum – ora pro
nobis) yaani msaada wa wakristu utuombee).
Mkristo ni mtu Yule
aliyemfasi wake Kristo kwa Ubatizo, hivyo tunaalikwa kumkimbilia mama yetu kwa
kusali Rozari kwa mama aliye msaada wetu katika maisha. Yeye alipokea ujumbe wa
Mungu kutoka kwa malaika nasi hatuna budi kupokea ujumbe mama anaotuletea
kutoka kwa mwanae. Mpendwa Mama Maria alizaliwa kipindi ambacho wazo la Malaika
lilikuwa la kawaida sana. Aliamini kuwa walijitokeza katika historia ya
wayahudi mara kwa mara. Malaika hawa walisaidia katika kutunga sheria (Matendo
7:38, Galatia 3:19) na kulinda waamini ( Kujtooka 23: 20; 2Kgs)
Kumwomba mama ni katika
Rozari Takatifu. Mpendwa Rozari ni sala ama tungo la sala ambamo sala ya ‘Baba
yetu’ na sala ya ‘atukuzwe Baba’ husaliwa mara kumi na tano kila moja na ile
sala ya maamkio ya malaika husaliwa mara mia moja na hamsini. Kwa sla hiyo
waamini hufundishwa jinsi ya kumheshimu mkombozi wetu kwa kuyawaza matendo
makuu kumi na matano ya maisha yake nay a mama yake.
Rozari ni injili kwa ufupi,
ni historia ya maisha ya Yesu Kristu. Katika ibada hii ya Rozari lengo kubwa
kwa mwaamini ni sharti daima liwe katika kuyaatafakari matendo haya; kumrudia
Mungu sifa na shukrani kutokana na matendo haya. Matendo haya ya Rozari
yanapaswa kuwa kiini cha mawazo ya mwamini kwa kuyaimarisha mapendo yake na
kuurekebisha mwenendo wa maisha yake kadiri yanavyovuta moyo wake. Sala ya
Rozari ni rahisi kusalika na kila mtu;zaidi ya hayo ni sala iliyo maarufu sana.
Mwaka 1572, papa aliwaamuru
waamini waitukuze kila mwaka sikukuu ya Bikira Maria mama wetu mshindi ili
kumwomba Mungu huruma yake kwa Kanisa na kwa ajili ya waamini wote,na
kumshukuru kwa ulinzi wake hasa kwa kuliokoa Kanisa kutoka katika mikono ya
waturuki waislamu waliotaka kuliangamiza.
Ndugu yangu ushindi huo
katika vita vya baharini vilivyopiganwa huko Lepanto(Ugiriki) ulionekana kuwa
umepatikana kutokana na sala na maandamano ya vyama vya rozari mjini
Roma,yaliyofanywa wakati wa mapigano hayo ya Lepanto.
Kumbukumbu hii inawahimiza
waamini wote kufanya fikara juu ya mafumbo ya Kristu kwa kufuata mfano wa
Bikira Maria ambaye kwa namna ya pekee alihusika na kuzaliwa, kuteswa na
kufufuka kwa mwana wa Mungu.
Hakuna mwanadamu yeyote
ambaye ameshawahi kumtumia rafiki yake maua ya aina ya miwaridi bila kuwa na
upendo naye. Ndiyo maana jamii ya wanadamu wanalinganisha ua hilo na upendo.
Wapagani kwa upande wao wanavika sanamu zao na miwaridi kama ishara ya upendo
unaobubujika kutoka katika mioyo yao.
Waamini wa mwanzo walifanya
tofauti kwa kufanya sala zao zichukue nafasi ya miwaridi. Nwa ndio maana leo
hii tunasikia watu waliotoa maisha yao kwa sababu ya kumtetea Kristo. Je! Leo
hii kulikoni? Mabikira wa kipindi hicho walivalia kanzu ndefu wakiwa wamevalia
taji la miwaridi kichwani walienda kumsalimu mfalme wa wafalme ambae kwa jina
lake watakufa. Waamini usiku walikusanya miwaridi hiyo na kuombea kila moja,
yaani waridi moja kwa sala moja. Wakazi wa jangwani huko Misri
(Egypt)-Waankorite na wahermit pia walikuwa na njia yao ya kuhesabu sala zao.
Walichukua mbegu za mazao au vijiwe
vidogo vidogo vilivyokusanywa pamoja na kutengeneza taji na utamaduni huu
Mohamedi aliuchukua kwa waislamu na mkusanyo wa miwaridi hii iliitwa
Rozari. Kwani rozari inamaanisha ( taji
la miwaridi). Kila sala zinaseemwa kwa kila waridi haikuwa hiyo hiyo kila
wakati walikuwa wanabadilisha badilisha. Kwenye Kanisa la Mashariki kulikuwa na
Rozari iliyoitwa Acathist (Akatisti) ambayo ni utenzi wa kiliturujia uliyo
saliwa katika hali tofauti tofauti bila kukaa. Sala hizi zililkuwa na mlolongo
mrefu wa wasifu wa mama Bikira Maria kuanzia mwanzoni mwa maisha ya Bwana wetu
Yesu Kristo.
Mt. Brigita alitumia rozari
iliyoundwa na salamu Maria na Baba yetu na mwishoni rozari ambayo tunatumia leo
ikatokea. Tunaambiwa mama Bikira Maria alimtokea Mt. Brigita karibu na kitanda
chake akamvika kichwani taji zuri. Huu ni mfano wa Rozari kama tuijuavyo leo
hii.
Mwanzoni kabisa Kanisa
liliwaasa waamini wake kusali zaburi zote 150 na utamaduni umeendelea hadi leo
kati ya mapadre wanaosali Zaburi hizi kila siku. Mpendwa haikuwa rahisi kwa
yeyote kukariri zaburi hizi 150. Pia kabla ya utaalamu wa uchapishaji ilikuwa
vigumu sana kutoa kitabu. Na hii ndiyo sababu vitabu muhimu kama Biblia
vilionekana na watu kama kitabu cha posta kilichounganishwa na simu nyingi za
watu hivyo hakikuvutia,hivyo watu walichoka kukitumia na baada ya hapo
likatokea jambo la ufinyu wa mawazo eti Kanisa lilikataza watu kusoma Biblia
kwasababu ilikuwa imeunganishwa unganishwa lakini ni kitabu ambacho hutumika sana
kama rejea ya simu za watu mbalimbali katika utamaduni wetu wa kileo.
0 comments:
Post a Comment