MATANDA RICHARD- MWANAMARIA
DHIMA YA BIKIRA
MARIA KATIKA MPANGO WA WOKOVU INAONESHWA WAZIWAZI KATIKA MAANDIKO MATAKATIFU.
Maandiko
Matakatifu ya Agano la Kale naya Jipya na Mapokeo ya kale yaonyesha wazi zaidi na zaidi
dhima(KAZI) ya Mama wa Mwokozi katika mpango wa wokovu, na kuiweka mbele yetu
tuifikirie. Vitabu vya Agano la Kale vyaeleza historia ya wokovu ambavyo ndani
yake hutayarishwa polepole ujio wa Kristo ulimwenguni. Maandiko hayo ya Kale,
yanavyosomwa katika Kanisa na kufahamika katika mwanga wa ufunuo kamili wa
baadaye, hatua kwa hatua yabainisha zaidi na zaidi sura ya yule mwanamke aliye
Mama wa Mkombozi. Katika mwanga huu anabashiriwa kinabii katika ahadi ya
ushindi juu ya nyoka waliyopewa wazazi wa kwanza baada yakutenda dhambi (taz.
Mwa 3:13).
Vilevile
yeye ni Bikira yule atakayepata mimba na kumzaa Mtoto mwanamume ambaye jina
lake ataitwa Emanuel CHUKUA BIBLIA YAKO UFUNGUE
KITABU CHA NABII Isa 7:14; Mik 5: 2-3; Mt. 1:22-23). Yeye anashika nafasi ya
kwanza miongoni mwa wanyenyekevu na maskini wa
Bwana,ambao,
kwa matumaini ya imani wanangojea na wanapata wokovu kwake. Hatimaye kwa yeye,
Binti mtukufu wa Sayuni aliye bora sana, baada ya kungojea kwa ahadi kwa muda
mrefu, nyakati zilitimia na mpango mpya wa wokovu ukawekwa, hapo Mwana wa Mungu
alipotwaa maumbile ya kibinadamu kutoka kwake, ili amkomboe mwanadamu katika
dhambi kwa mafumbo ya mwili wake.
Mungu
wa huruma alitaka Umwilisho utanguliwe na ukubali wake yeye aliyeteuliwa tangu
milele awe Mama, ili kama vile mwanamke alivyoshiriki kuileta mauti, kadhalika
mwanamke asaidie kuuleta uzima. Hayo yamhusu kwa namna ya pekee Mama wa Yesu aliyeuzalia ulimwengu Uzima wenyewe,
utengenezao yote upya, naye alitajirishwa na Mungu kwa karama zenye kustahili
jukumu hili kubwa hivi. Kwa hiyo
hatuwezi kushangaa ikiwa Mababa Watakatifu walizoea kumwita Mama wa Mungu kuwa “ Mtakatifu
kabisa”, bila doa lolote la dhambi
kama alivyotengenezwa na Roho Mtakatifu
na kufanywa kuwa kiumbe kipya (176) Hali
amepambwa tangu nukta ya kwanza ya kutungwa kwake mimba kwa kwa mng’aro wa
utakatifu wa pekee kabisa, Bikira huyu wa Nazareti aliamkiwa na Malaika mhubiri (Angelo nuntiante), Kwa amri
ya Mungu kuwa “ Mtakatifu kabisa” kwa amri ya Mungu, kuwa “amejaa neema”(Gratia plena)
Soma injili ya.Lk 1:28 naye akamjibu mjumbe
huyu wa mbinguni “Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana na iwe kwangu kama ulivyosema” (Lk
1;38). Hivyo Maria, binti Adamu, kwa
kulikubali Neno la Mungu amekuwa
mama waYesu, na akiyakumbatia kwa
roho yake yote, na bila kushikwa na dhambi yoyote, mapenzi ya Mungu
yenye wokovu, akajitoa kabisa kama mjakazi wa Bwana kwa ajili ya nafsi ya
Mwanawe na kwa kazi yake, akilihudumia fumbo
la ukombozi chini yake na pamoja naye kwa neema ya Mungu Mwenyezi. Kwa
hiyo Mababa Watukufu huona kwa haki kuwa Maria hakutumiwa na Mungu katika hali
ya kutendwa tu, bali alishiriki kuleta wokovu wa binadamu kwa imani yake na
utii wake wa hiari.
Ndiyo sababu, Mababu wa Kanisa wasio wachache
hupenda kueleza katika mahubiri yao kwamba “Fundo la kutotii kwa Hawa(EVA)
limefunguliwa kwa utii wa Maria; na kile ambacho Hawa alifunga kwa kutosadiki kwake, Bikira Maria
alikifungua kwa imani yake”(178).Wakimfananisha [ Maria] Hawa, wanamwita Maria
“Mama wa walio hai na mara nyingi wanakitangaza
maneno “Mauti yalikuja
ulimwenguni kwa njia ya Hawa na uzima
umeingia ulimwenguni kwa njia ya Maria ”
Umoja huu wa Maria na Mwanawe katika kazi ya
wokovu unaonekana tangu dakika ile
Bikira alipotunga mimba ya Kristo mpaka kifo chake. Kwanza Maria alipoondoka
kwenda kwa haraka kumwamkia Elisabeti
akasalimiwa naye kuwa mwenye heri kwa imani yake katika wokovu
ulioahidiwa, na mtangulizi akaruka ndani ya tumbo la mama yake fungua Biblia
yako injili ya Luka Lk 1: 41-45 tena,
wakati wa kuzaa, Mama wa Mungu alipowaonyesha wachungaji na mamajuzi kwa
furaha Mwana wake mzaliwa wa kwanza asiyepunguza ukamilifu wa ubikira wake bali
akautakatifuza (181) Na alipomtolea
Bwana hekaluni, pamoja na sadaka ya maskini alimsikia Simeoni akiagua
kwamba Mwanae atakuwa ishara itakayonenewa,
na kwamba upanga utaingia moyoni mwake mama ili yafunuliwe mawazo ya
mioyo mingi ( taz Lk 2:34-35)
Walipomkosa
mtoto Yesu na kumtafuta kwa huzuni wazazi wake wakamwona hekaluni
akiyashughulikia yale yaliyo ya Baba yake, wala hawakuelewa neno hilo la Mwana. Lakini mama yake aliyaweka haya
yote moyoni mwake akitafakari, fungua injili ya Lk 2:41-51)
Maria katika
maisha ya hadharani ya Yesu
Katika maisha ya hadharani ya Yesu, mama yake
alijionyesha tangu mwanzo kwa njia ya pekee katika arusi ya Kana ya Galilaya aliposababisha kwa huruma yake
chanzo cha ishara za Yesu aliye Masiya, kwa njia ya maombezi yake, (taz Yn 2:
1-11). Wakati wa kuhubiri kwake Mwanae alipokea maneno ambayo kwayo yeye akiuinua Ufalme juu ya
Maria baada ya kupaa kwake Bwana.
Kwa kuwa ilimpendeza Mungu sakramenti ya
wokovu wa wanadamu isidhihirishwe kitukufu kabla ya kumimina Roho aliyeahidiwa
na Kristo, tunawaona Mitume kabla ya
siku ya Pentekoste “wakidumu kwa moyo mmoja kaktka kusali, pamoja nao wanawake
na Maria, mama yake Yesu, na ndugu zake” (Mdo 1: 14). Hata Maria aliomba kwa
sala zake paji la Roho ambaye alimfunika
tayari kama kivuli siku ya kutangazwa kwake.
Mwishowe Bikira asiye na doa alikingiwa na
kila doa la dhambi ya asili, (183). Akishamaliza mwendo wa maisha yake duniani,
aliinuliwa katika utukufu wa mbinguni pamoja na mwili [wake] na pamoja na roho
[yake] (184) akatukuzwa na Bwana kama Malkia
wa ulimwengu, ili afananishwe kikamilifu na Mwanawe aliye Bwana wa
mabwana (taz. Ufu 19: 16) na mshindi wa dhambi na mauti(185).
0 comments:
Post a Comment