NI MAMA WA MUNGU, NI MAMA ALLIYEKINGIWA DHAMBI YA ASILI, NI BIKIRA DAIMA NA NI YULE ALIYEPALIZWA MBINGUNI MWILI NA ROHO. Waswahili wanamsemo wao wasemao kuwa Mti
wenye matunda ndio upigwao mawe. Mpendwa katika Kristu ukiwa mtu mwema
daima tarajia kupata makombora kutoka kwa majirani zako kwasababu ya wema wako.
Ukiona huna makombora yoyote kutoka kwa wenzako tambua unakasoro Fulani. Maria
mama yetu amekuwa akipata makombora
au mashambulizi kutoka kila
upande kuanzi kipindi kile cha kanisa la awali
ambapo mzushi mmoja Nestory alikataa kabisa Bikira Maria kuitwa mama wa
mungu. lakini hii kwa mtu anayefahamu
msemo huo ataacha kabisa kumsema mama
vibaya.
inawezekana kuwa Maria mama yetu anayetupenda akawa tena chanzo cha kujenga
ukuta kati ya wakatoliki na waprotestant? Swali hili nitalijibu tunavyoendelea.
Mwaka juzi mtu mmoja alitembelea nchi mbalimbali
duniani zikiwemo Kenya,Kongo, na Rwanda. Kila mahala alipokwenda aliulizwa
swali ni kwa namna gani watajibu waprotestant maswali wanayowatupia kuhusu
Bikira Maria.
Inaonekana leo hii katika vitabu mbalimbali vinavyo
chapishwa kumhusu Maria kwamba makanisa makubwa ya kiprotestant taratibu
yameanza kumtambua binti huyu wa Nazareth. Hii inatokana na tafakari yao juu ya
maneno yote aliyosema mwanzilishi wao Martin Luther. Ambaye katika uhai wake
alisema “maria ni kweli mama wa Mungu” na akawa anaimba nyimbo mbalimbali
zikiwemo za kumsifu mama kama vile SALVE
REGINA wimbo ulioimbwa hapo zamani na mwishoni mwa wimbo huu maneno “ BIKIRA MARIA yalisikika. Ndugu zangu
wimbo huu hata leo hii bado unasikika katika baadhi ya makanisa.
Sasa
tuangalie picha ya mama yetu ndani ya Biblia ambayo inawakilisha wakristo wote.
Mama huyu alimpenda Kristo mpaka akawa mfuasi wake na sasa kwa namna ya pekee yuko katika roho
ya kila Mkristo kama mwombezi wake. Wewe unayenisikiliza tambua kuwa mama yuko
tayari kukuombea anza sasa kama ulikuwa bado.
Ni kweli
kwamba waprotestant wanauliza wakatoliki maswahili mengi kwa kile wanachosema na kusikia kuhusu ibada
kwa Bikira Maria wanazofanya. Na
wakatoliki kwa upande wao nao huwauliza maswali waprotestant kuhusu unyamavu
wao juu ya sifa kemkem ambazo zinamhusu mama zilizoandikwa ndani ya Injili.
Sisi tunaomfahamu mama yetu tunaalikwa leo kujua
kuwa jina protestant ni mkusanyo wa makanisa mengi. Mfano waorthodox ambao si
wakatoliki lakini wanaonesha upendo wa pekee kwa mama ambao unafanana kwa
karibu sana na wa kikatoliki.
Waothodoxy
wanaenda mbali zaidi kuliko wakatoliki kwa namna wanavyo mheshimu B.M katika
tenzi zao na kwenye sikukuu zao mbalimbali zinazomhusu mama. Vipo viashiria
vingi katika makanisa yao vinavyoashiria jinsi mama alivyo mama wa Mungu (
theotokos).
Maria
alimpenda mwanae na akajitoa kabisa kwake. Kama
vile haikutosha anatupenda nasi pia kwa kuwa Kristo alitufikia kumpitia
mama Maria. Kama mama atafahamika vizuri na kazi zake atakuwa kwetu chanzo cha
umoja ingawa tuna utofauti wetu wa kikabila,kidini,kitaifa na kimazingira.
sasa tuangalie jinsi mama alivyokuwa mfuasi kamili wa mwanae. Mama
alikuwa wa kwanza kuinjilishwa habari njema na malaika Gabriel na alikuwa wa
kwanza kumfanya Kristo awe kitovu cha maisha yake. Nakualika umfanye sehemu ya
maisha yako nawe utabarikiwa sana.
Mpendwa mama maria ndiye aliyekuwa wa kwanza kusema ndiyo kwa Mungu,kule kukubali kuwa mama wa mungu. Na ndiyo yake hii
inakuwa mwanzo wa ndiyo zote wanadamu wanazoonesha kwa Mungu wao katika yote
watendayo. Ndiyo ya mama , ilitangulia ndiyo ya mtakatifu Yosefu aliyekubali
kumchukua na kumwacha kwa siri baada ya kuambiwa na malaika kwamba anaujauzito
kwa uwezo wa roho mtakatifu. Ndiyo yake inarithiwa kutoka kizazi hadi
kizazi,karne hadi karne na kutufanya tutoe ndiyo zetu mbele ya Mungu.
Kumpitia
mama, Kristo alipendwa mpaka watu walidhiriki kusema “heri maziwa aliyonyonya” jamani! Kumbe hata maziwa ya mama
yalibarikiwa! Sembuse utu wake mzima? Mama alibarikiwa sana amini hilo.
Mpendwa mama yetu alikuwa mmisionari wa kwanza. Alifunga safari kutoka
Nazareth mpaka AIN KARI akimbeba Yesu akipitia barabara zilizochongwa na
wanadamu mpaka kwenye familia ya mbatizaji. Na kupitia Elizabeth, mama yake Yohani
mbatizaji,familia hii ilikiri bila kusita imani ya Kikristu kwa kusema – mimi
ni nani hata mama wa Bwana wangu aje kwangu?. Mpendwa kila Mkristo wa kweli
anatambua kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Mpendwa kwa kuwa karibu
na mama, nawe utakuwa mzazi wa Yesu na daima utambeba daima katika moyo wako na
daima utachagua mema kama mama alivyofanya.
Mmisionari
wa jana, leo na kesho wote wanafuata nyayo za mama kwa kumbeba Kristo na
kumpeleka kwa wahitaji.
Je! unaelewa
mtu wakwanza kubarikiwa katika Injili , ni
mama yetu Bikira Maria na akawa wakwanza kutangazwa mwenye furaha kwa
sababu ya imani yake . hivi nikuulize umeshawahi kufurahi kwasababu ya imani
yako? Kama sivyo ni kwa nini? Jifunze
leo kutoka kwa mama aliyetanganzwa kuwa mtu wa kwanza kusifiwa kwasababu ya
imani yake.
endelea kusoma mafunzo haya kwa upanuzi zaidi wa uelewa wako. kuhusu mafunzo sahihi ya Kanisa kujhusu mama yetu Bikira Maria.
ReplyDelete