Home » » HUYU NDIYE NKEREKETWA WA BIKIRA MARIA

HUYU NDIYE NKEREKETWA WA BIKIRA MARIA







Huyu ndiye Padre RICHARD MATANDA TESHA wa Jimbo katoliki Moshi. Alizaliwa
Tarehe ya  26/06/1972.na  ni mzaliwa wa Parokia Ya Uru– Shimbwe.

Baada  ya masomo yake ya Msingi alijiunga na seminari ya Mt.Yakobo “St. James
seminary” mwaka 1991– 1996

Na hatimaye masomo ya falsafa (Philisophy) katika chuo  cha Kibosho– Moshi
 kwa miaka mitatu. Na hatimaye Masomo ya teolojia ( huko Segerea Dar-Es-Salam.)
 Na kwa miaka niwili chuoni Mwanza  SAUT akisomea
 mawasilianoya jamii na masoko. Tuzidi kumwombea kwa changamoto mbalimbali
anazokumbana nazo katika utume wake ili azidi kumhubiri Kristo msulubiwa.

Mwandishi huyu  amekuwa akijituma katika  kuandika vijitabu mbalimbali kuhusu
mama yetu mpendwa Bikira Maria na kutoa tafakari mbali mbali
katika taasisi na kwenye vyombo vya habari hasa Redio Maria. na Redio SAUT ya
Jijini Mwanza.

ameandika vitabu mbalimbali kama:TAFAKARI NA PADRE
MATANDA, cha pili JE! UNAMJUA HUYU na cha tatu  MSAMAHA
 ISHARA YA UPENDO ambacho amekiandika akiwa Huruma Hosptal Januari hadi
  Febrari 2014 .

Padre Richard Matanda Tesha anatumia mang’amuzi aliyoyapata shuleni katika
 Masomo yake ya Philosophy na Theology na tafakari zake binafsi ili kuelimisha jamii. kwa sasa anapatikana Mango Parish kuanzia 12/03/2014

  

0 comments:

Post a Comment

RICHARD MATANDA TESHA

 
Support : Richie | Bikira Maria | Elimu Endelevu
Copyright © 2013. BIKIRA MARIA - All Rights Reserved
Template Created by Mwariko Published by Mwariko team
Proudly powered by Jicho la Habari