MARIA ANAZUNGUMZA NAWEWE
Kila kitu ninachokushirikisha mwanangu mpendwa, si chako peke
yako bali ni kwa wanangu wote ninaowapenda kupita kila kitu. Ujumbe huu ni kwa
wote wanaompenda mama yetu mpendwa Bikira Maria. Ubaki daima katika moyo wangu na kuwa mwaminifu kwangu mwanangu.
1.
Nitakuwa daima nawe.
Weka maazimio yako kwa moyo wangu
safi, wewe ni wangu na mali yangu.
Kila muda au wakati uwe kama
ninavyopenda,fanya ninavyopenda. Usiogope kwani nitakuwa karibu nawe. Niko kwenye
harakati za kukuandalia mambo makuu zaidi lakini kidogo kidogo kama mama anavyo
mfanyia mwanae.
2. Utume wako
Leo ninafuraha kubwa sana nawe kwani
umekaa karibu sana na moyo wangu. Unaona vitu vya ulimwengu huu jinsi vilivyo mbali nawe na visivyo vya
kueleweka mbele yako. Unatazama na kuona vitu hivyo vinavyokuchosha ambavyo si
mimi mama yako ninayekupenda kama
ulivyo.
Jifunze kupagawa nami ili kila kitu ufanyacho, nitakuwa
ni mimi ninayefanya kukupitia wewe. Na ninapenda kutenda kukupitia wewe.
Utateseka sana lakini jipe moyo kwani daima nitakuwa nawe.
3. Sababu ya machozi yangu
Nimefarijika sana asubuhi ya leo. Ulipokuwa
unatazama sanamu yangu inatoa machozi na pia umekuja misa ili kuufariji moyo
wangu safi. Nimefurahia mawazo yako ya uwana na upendo. Ni kweli nimefarijika
Machozi yangu ni kwa sababu ya watoto
wangu wasio mjali Mungu tena na kujizamisha katika furaha za ulimwengu huu.
Nalia pia kwa ajili ya wanangu mapadre ambao hawanijali tena, wanakufuru na
kumwacha mwanangu peke yake kwenye tabernakulo. Kila mmoja nampenda kivyake .
nakuomba uwaombee hawa mapadre kwani wao wamekabidhiwa dhamana kubwa ya
kuwaokoeni.
4. Nitakuwa kiongozi wako
Natambua kabisa unajiona kuwa hufai
kwa utume wangu na kuniuliza kwanini “ hukuchagua mtu mwingine
anayefaa na mwenye uwezo?” na kwa nini unanitegemea na unajua madhaifu yangu yaliyopita?
Mwanangu nimekuchagua kwa sababu ya
udhaifu wako na hakuna mtu atakayesema kuwa hii ni kazi yako. Nitadhihirisha
uwezo wangu kutokana na udhaifu wako.
Kwa utupu wako kiakili nitadhihirisha uwezo wangu. Mimi mwenyewe nitakuwa
kiongozi wa jeshi langu. Kusiwepo na kiongozi mwenu mimi nitaongoza yote.
Kitu cha pekee ninachotaka kutoka
kwako ni kukubali uongozi wangu kwa moyo wako wote kama vile mwanangu alivyojitoa
kabisa kwangu na kuniamini ndipo nitakuwa mlinzi wa kila kitu katika maisha
yako.
5. Acha mimi niwe mtendaji.
Kwanini unahangaika na kuwa na
wasiwasi? Tambua unaongozwa na mimi. Kujitolea kabisa kwangu kuna maanisha
kujiachia kabisa kwangu nikuongoze kama vile mtoto alivyo kwa mama yake.
6. Mimi daima ni mama.
Je! Unapendezwa na nyumba
ninayokutengenezea? Hujawahi kuota kuwa itakuwa hivyo kwenye pango katika
miamba.. najua hukuwa na habari kwamba
nilikuwa nakuandalia nyumba hiyo. Ulipokuwa unatenda kwa ajili yangu, ukiteseka
kwa joto na uchovu, ungeweza kusema ‘ni furaha iliyoje kufanya kwa ajili ya
mama yangu mpendwa Maria. Nilikuwa nakufikiria na kukuandali mahali pa
kupumzika. Nimekuleta mahali hapa nikijua ni pazuri kwako na kwangu. Kuna
mwingine anaye nipenda sana. Kuna watoto wengine wengi wanaonipenda. Wewe ni
mojawapo wa hao wanaonipenda.
7. Uwe mwangalifu na mwenye kusali
Wako mapadre ambao wameacha ujumbe wa
injili na kung’ang’ania malimwengu na kujikita zaidi katika utajiri. Ni kwa
sasbabu hii ulimwengu utaangamia kwa sababu yao. Ni wanangu nyie mnaonipenda
ambao mtakaoleta mageuzi katika ulimwengu huu. Nami nitakuwa pamoja nawe katika
dhoruba zinazokusonga.
8. Mioyo ya mapadre wangu
Uwe nami moyonni kila mara utapata amani. Usihofu kwa ajili ya lipi
utakalofanya. Yule ambaye amejitolea kwangu , ni wa kwangu kabisa na hawezi
kabisa kuchagua yeye binafsi anachotaka kufanya. Ukibaki ndani mwangu
nitakwambia kipi cha kufanya kwa wakati husika.
Nimekupokonya mikononi mwa maadui wangu sasa umechukua njia kuelekea
fadhila ya upendo, ili chochote kifanyike kadri ya matakwa yangu. Nitakushika
mkono na tutafanya yote pamoja. Nakuonea wivu
kwa kuwa name mama yako mpendwa.
Wambia kwamba nataka kitu kimoja kutoka kwao yaani kujitoa kabisa kama
watoto wangu,wakiachilia yote kwangu kiwe kizuri au chenye heshima na kunipa
mioyo yao. Ndipo nitakapokuwa mama yao sawa sawa.: msomaji unaweza kutoa maoni yako kwa ajili ya kuboresha
0 comments:
Post a Comment