Mpendwa nakukaribisha katika kipindi hiki cha elimu juu ya Bikira Maria
ambacho kitakueleza mengi kumhusu mama yetu B.Maria na jinsi maandiko
matakatifu na kanisa vinavyosema juu yake. Ninaekuletea kipindi hiki ni
mimi Padre Richard Joseph Matanda Tesha wa jimbo katoliki la moshi
Mpendwa kuna kila sababu wewe na mimi kujua maada hii juu ya mama yetu
mpendwa B.Maria. kanisa letu limekuwa na utamaduni uliojengwa juu ya
Ibada kwa B.Maria tangu zamani kwa kuwa yeye ndiye mama wa Mkombozi
wetu. Mama huyu anatuelekeza kwa kristu na tunathubutu kusema “kumjua
mama B.Maria ni kumjua Kristo Yesu. Hii ni kwasababu yeye alimuiga
kisawasawa naye ni mfano bora wa kuigwa na wakristo wote na Kanisa kwa
ujumla.
0 comments:
Post a Comment