Home » » WASIFU WANGU

WASIFU WANGU

mimi ni Padre Richard Joseph Matanda Tesha, mzaliwa wa parokia ya uru shimbwe Moshi- kilimanjaro. Nimefanya utume wangu katika parokia za Kirua,Makomu Marangu, seminari ya St. James kama mwalimu wa kiswahili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tano na General studies form five na six. Nimekuwa Kapilano wa masisita novisiati maili sita.

Nilienda masomoni mwanza nikasoma kwa miaka miwili tu mawasiliano ya jamii na masoko (public Relations and marketing). utume wangu katika parokia ya Olele Rombo na hatimaye Mango Kibosho.

Nimekuwa mkereketwa wa kumwinjilisha mama yetu Bikira Maria katika semina mbalimbali na kwenye  vyombo vya habari kama radio Maria ya jijini Dar-es-Salam.

Napendelea sana kufunga na kusali- licha ya changamoto mbalimbali ninazo kumbana nazo. nakuomba uniombee sana kwa Mungu, ili niweze kutekeleza majukumu yangu haya.

0 comments:

Post a Comment

RICHARD MATANDA TESHA

 
Support : Richie | Bikira Maria | Elimu Endelevu
Copyright © 2013. BIKIRA MARIA - All Rights Reserved
Template Created by Mwariko Published by Mwariko team
Proudly powered by Jicho la Habari