Home » » MPASUKO

MPASUKO


BIKIRA  MARIA  MSAADA WA  WATU. (ADIUTRICEM POPULI – HELPER OF THE PEOPLE)

Tarehe 5/9/1895 baba mtakatifu Leo XIII alitoa waraka wake wakichungaji kuhusu Rozari wenye kichwa cha habari “ msaada wa watu”- Adiutricem Populi. Katika waraka wake huu aliwaasa waamini kusali Rozari kwa mama yetu mpendwa aliye mama wa Kanisa. Anatoa sababu ya kumwita Bikira Maria mlinzi wa wanakanisa. Maria alikuwa na wajibu wa kuwafanya wanakanisa kuwa wamoja na kuimarisha imani ya kanisa. Wakati Yesu alipopaa mbinguni mama alibaki hapa duniani kuongoza hatua za awali kabisa za kanisa na kuwatia moyo mitume kwa kazi yao ya kuenezan Injili. Na alipopalizwa mbinguni anaendelea na amefanya hivyo mara nyingi katika historia ya kanisa alivyoingilia mambo mbalimbali ili kuamsha imani ya waamini na kuepuka uzushi mwingi uliokuwa unaenea kila mahala.
Baba mtakatifu aliendelea kussema watu waendelee kusali kwani kwa msaada wa mama, makanisa ya mashariki yatarudi katika kundi moja. Katika mtaguso waw Efeso, wakristo wa mashariki na magharibi walijumuika pamoja katika umoja mbele ya Bikira Maria katika ibada moja. Ndio maana ibada ya mama yetu inatiliwa sana maanani kwani huleta watu pamoja.
Baba huyu mtakatifu Leo XIII aliwaalika wakristu wote kumwomba sana huyu mama Bikira Maria ili kuweza kuleta pamoja watoto wake wote katika kanisa moja. Ndiyo maana mpendwa mwanafamilia tunaposali litania ya Bikira Maria tunasali (Auxilium christianorum – ora pro nobis) yaani msaada wa wakristu utuombee).
Mkristo ni mtu Yule aliyemfasi wake Kristo kwa Ubatizo, hivyo tunaalikwa kumkimbilia mama yetu kwa kusali Rozari kwa mama aliye msaada wetu katika maisha. Yeye alipokea ujumbe wa Mungu kutoka kwa malaika nasi hatuna budi kupokea ujumbe mama anaotuletea kutoka kwa mwanae. Mpendwa Mama Maria alizaliwa kipindi ambacho wazo la Malaika lilikuwa la kawaida sana. Aliamini kuwa walijitokeza katika historia ya wayahudi mara kwa mara. Malaika hawa walisaidia katika kutunga sheria (Matendo 7:38, Galatia 3:19) na kulinda waamini ( Kujtooka 23: 20;  2Kgs)
Kumwomba mama ni katika Rozari Takatifu. Mpendwa Rozari ni sala ama tungo la sala ambamo sala ya ‘Baba yetu’ na sala ya ‘atukuzwe Baba’ husaliwa mara kumi na tano kila moja na ile sala ya maamkio ya malaika husaliwa mara mia moja na hamsini. Kwa sla hiyo waamini hufundishwa jinsi ya kumheshimu mkombozi wetu kwa kuyawaza matendo makuu kumi na matano ya maisha yake nay a mama yake.
Rozari ni injili kwa ufupi, ni historia ya maisha ya Yesu Kristu. Katika ibada hii ya Rozari lengo kubwa kwa mwaamini ni sharti daima liwe katika kuyaatafakari matendo haya; kumrudia Mungu sifa na shukrani kutokana na matendo haya. Matendo haya ya Rozari yanapaswa kuwa kiini cha mawazo ya mwamini kwa kuyaimarisha mapendo yake na kuurekebisha mwenendo wa maisha yake kadiri yanavyovuta moyo wake. Sala ya Rozari ni rahisi kusalika na kila mtu;zaidi ya hayo ni sala iliyo maarufu sana.
Mwaka 1572, papa aliwaamuru waamini waitukuze kila mwaka sikukuu ya Bikira Maria mama wetu mshindi ili kumwomba Mungu huruma yake kwa Kanisa na kwa ajili ya waamini wote,na kumshukuru kwa ulinzi wake hasa kwa kuliokoa Kanisa kutoka katika mikono ya waturuki waislamu waliotaka kuliangamiza.
Ndugu yangu ushindi huo katika vita vya baharini vilivyopiganwa huko Lepanto(Ugiriki) ulionekana kuwa umepatikana kutokana na sala na maandamano ya vyama vya rozari mjini Roma,yaliyofanywa wakati wa mapigano hayo ya Lepanto.
Kumbukumbu hii inawahimiza waamini wote kufanya fikara juu ya mafumbo ya Kristu kwa kufuata mfano wa Bikira Maria ambaye kwa namna ya pekee alihusika na kuzaliwa, kuteswa na kufufuka kwa mwana wa Mungu.
Hakuna mwanadamu yeyote ambaye ameshawahi kumtumia rafiki yake maua ya aina ya miwaridi bila kuwa na upendo naye. Ndiyo maana jamii ya wanadamu wanalinganisha ua hilo na upendo. Wapagani kwa upande wao wanavika sanamu zao na miwaridi kama ishara ya upendo unaobubujika kutoka katika mioyo yao.
Waamini wa mwanzo walifanya tofauti kwa kufanya sala zao zichukue nafasi ya miwaridi. Nwa ndio maana leo hii tunasikia watu waliotoa maisha yao kwa sababu ya kumtetea Kristo. Je! Leo hii kulikoni? Mabikira wa kipindi hicho walivalia kanzu ndefu wakiwa wamevalia taji la miwaridi kichwani walienda kumsalimu mfalme wa wafalme ambae kwa jina lake watakufa. Waamini usiku walikusanya miwaridi hiyo na kuombea kila moja, yaani waridi moja kwa sala moja. Wakazi wa jangwani huko Misri (Egypt)-Waankorite na wahermit pia walikuwa na njia yao ya kuhesabu sala zao. Walichukua mbegu za mazao au  vijiwe vidogo vidogo vilivyokusanywa pamoja na kutengeneza taji na utamaduni huu Mohamedi aliuchukua kwa waislamu na mkusanyo wa miwaridi hii iliitwa Rozari.  Kwani rozari inamaanisha ( taji la miwaridi). Kila sala zinaseemwa kwa kila waridi haikuwa hiyo hiyo kila wakati walikuwa wanabadilisha badilisha. Kwenye Kanisa la Mashariki kulikuwa na Rozari iliyoitwa Acathist (Akatisti) ambayo ni utenzi wa kiliturujia uliyo saliwa katika hali tofauti tofauti bila kukaa. Sala hizi zililkuwa na mlolongo mrefu wa wasifu wa mama Bikira Maria kuanzia mwanzoni mwa maisha ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Mt. Brigita alitumia rozari iliyoundwa na salamu Maria na Baba yetu na mwishoni rozari ambayo tunatumia leo ikatokea. Tunaambiwa mama Bikira Maria alimtokea Mt. Brigita karibu na kitanda chake akamvika kichwani taji zuri. Huu ni mfano wa Rozari kama tuijuavyo leo hii.
Mwanzoni kabisa Kanisa liliwaasa waamini wake kusali zaburi zote 150 na utamaduni umeendelea hadi leo kati ya mapadre wanaosali Zaburi hizi kila siku. Mpendwa haikuwa rahisi kwa yeyote kukariri zaburi hizi 150. Pia kabla ya utaalamu wa uchapishaji ilikuwa vigumu sana kutoa kitabu. Na hii ndiyo sababu vitabu muhimu kama Biblia vilionekana na watu kama kitabu cha posta kilichounganishwa na simu nyingi za watu hivyo hakikuvutia,hivyo watu walichoka kukitumia na baada ya hapo likatokea jambo la ufinyu wa mawazo eti Kanisa lilikataza watu kusoma Biblia kwasababu ilikuwa imeunganishwa unganishwa lakini ni kitabu ambacho hutumika sana kama rejea ya simu za watu mbalimbali katika utamaduni wetu wa kileo.

0 comments:

Post a Comment

RICHARD MATANDA TESHA

 
Support : Richie | Bikira Maria | Elimu Endelevu
Copyright © 2013. BIKIRA MARIA - All Rights Reserved
Template Created by Mwariko Published by Mwariko team
Proudly powered by Jicho la Habari