Maria
alipendelewa na Mungu kwasababu alimchagua kuwa mama wa mtoto wake ambae
atakuwa mkombozi wa dunia nzima atakayemwokoa mwanadamu kutoka mitego ya
shetani na dhambi.
Maandiko matakatifu yanatuambia kuwa mama huyu amejaa
neema na Mungu yuko pamoja naye (Lk 1:28) salamu hii ya malaika Gabriel inakuwa
chanzo cha sala zetu ( salamu Maria umejaa neema Bwana yu nawe umebarikiwa
kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa,maria mtakatifu
mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu amina.) mpendwa
nakualika kuisali sala hii kwa utulivu na kutafakari kila unachokisema. Tunaona
hapa kwamba Mungu alipaanda mahali pa kuishi katika harakati za kuanza
ulimwengu mpya uliokombolewa.
Wanateolijia
na baba watakatifu ambao walihusika sana katika kuanda misingi imara juu ya
mama yetu. Ukweli kwamba yeye alikingiwa dhambi ya asili anakuwa kiumbe cha juu
sana kupita vyote vinavyozaliwa na dhambi ya asili. Mt. Thomas wa Akwino
alisema kwamba kila kilicho kikamilifu kinapatikana katika nafsi ya B.Maria. na
kila kitu ambacho watakatifu wanacho kama karama yao mama Bikira anacho kwa
ukamilifu wake( mf. Kama mtakatifu Fulani alikuwa mpenda watu sana mama bikira
maria anakipaji hicho kwa ukamilifu wake).
Mama Bikira Maria ana ukaribu wa pekee na
mwanae(Bwanawetu Yesu Kristu).Ikiwa na maana kuwa alishirikiana na
anashirikiana na mwanae katika kazi ya kumkomboa mwanadamu. Alishirikiana naye
kwa kila hali katika harakati za kumkomboa mwanadamu. Mama huyu anasimama
kinyume na Eva mwanamke wa kwanza na mama wa wote wenye mwili. Kila kilichopotea
kwa ajili ya Eva kimerudishiwa hadhi yake na B.Maria. mt. Augustino
alithibitisha ukweli huu aliposema “Hapa tunagundua fumbo kubwa;kwamba katika
mwanamke tunakufa na katika mwanamke tunarudishiwa uzima”. Na kwa hali hiyo
kutokana na imani yetu ya kikatoliki tunapata kujua kuwa kufanyika mtu kwa
mwana wa Mungu au kuja kwa mkombozi kuna uhusiano na dhambi ya asili anguko la
wazazi wetu wa kwanza(Adamu na Eva)
mfanye mama huyu kuwa mwombezi wako. alifanya mengi katika harakati ya ukombozi wako. asiye sikia la mkuu huvunjika guu. says fr. matanda
ReplyDelete