Ili mwana
wa Mungu kuwa mwanadamu na kutukomboa ,nafsi ya pili ya utatu mtakatifu
alipaswa kuwa na mama wa kibinadamu ambaye ni B.Maria. sasa naomba tuangalie
hatua ambazo Mungu alizichukua ili kumpata mama wa Mkombozi.
Lengo la
mwokozi ni kumkomboa mwanadamu kutoka utumwa wa shetani na dhambi,na haingekuwa
jambo jema mkombozi ahusike na dhambi kwa nanma yoyote. Ndiyo maana tunasema
yeye alikuwa mwanadamu kama sisi isipokuwa hakuwa na dhambi. Kutokana na muono
huo wa Mungu,alimkinga B.Maria na dhambi ya asili. Mpendwa bilashaka unajua
kuwa kila mwaka tunasherekea sikukuu ya B.Maria Mkingiwa dhambi ya asili tarehe
8/12 kila mwaka; sina uhakika kama baadhi yetu leo hii tunatambua sherehe hii
na maana yake. Kuna kipindi katika historia ya kanisa ambapo dalili za kuelewa
sikukuu hii inajiodhihirisha lakini leo hii wapo wengi wasiotambua na ndio
maana ifikapo sikukuu hii hata kwenda kanisani inakuwa shida sana. Tuaalikwa
kujirudi na kutambua tunu zetu katika imani yetu.
Funzo imani
hili juu Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili lilitangazwa na Baba mtakatifu
Pius IX huko Roma tarehe 8/12/1854. Funzo hili
linamaanisha kuwa Bikira Maria alikingiwa na dhambi ya asili kuanzia
pale alipotungwa mimba. Mama yetu mpendwa Bikira Maria allizaliwa kama wanadamu
wengine wazazi wake wakiwa Anna na Joachim.
Mpendwa,ili
kuelewa kanisa linamaanisha nini na fundisho hili,ni vizuri kukumbuka kuwa
Neema ya utakaso kabla ya anguko lao. Hawa ndio wazazi wetu wa kwanza kabisa.
Adamu hakuwa tu baba yetu alikuwa pia kioo cha maadili ya jamii ya wanadamu na
Mungu alimjaribu, hapa namaanisha kuwa angerithisha kwa watoto wake neema
aliyokuwa nayo kama angekuwa mtii kwa Mungu aliyemuumba. Hivyo kuwa na Neema
hiyo ya kimungu au kukosa neema hiyo kulitegemea sana utii na uaminifu wa Adamu baba yetu kwa Mungu baba
yetu.
Msikilizaji
mpendwa,sote tunaelewa kilichotokea. Adamu alitenda dhambi na akapoteza neema
si kwake tu lakini nasi sote tukaikosa kwa sababu yeye alituwakilisha sote.
Ndiyo maana tunazaliwa tukiwa tuanakosa vitu ambavyo tungepaswa kuwa navyo kama
neema ya Mungu. Mama kanisa anaita hali hii “ dhambi ya asili”. Lakini kwa
neema yake Kristu aliturudishia neema tuliyoipoteza kwa maisha yake,mateso na
kifo na kwa njia ya ubatizo tunarudishiwa mema ya kimungu na kuwa watoto wa
Mungu na warithi wa mbinguni.
Dhambi ya
asili inaelezeka kama kujitenga na Mungu na kuwa katika utumwa wa Yule mwovu.
Kutokana na ukweli huu wababa wakanisa wanajiuliza hivi inawezekanakweli kuwa
Bikira maria ilikuwa mtumwa wa shetani hata mara moja? Lahasha !Walivyotafakari
kwa kina sana jambo hili walifikia hatua ya kusema Mama Bikira maria alikingiwa dhambi ya asili. Maandiko matakatifu
yanaashiria jambo hili la kukingiwa dhambi ya asili ingawa si kwa uwazi kabisa.
Mara tatu hivi wababa wanatumia maneno yafuatavyo kama kiashiria’ kitabu cha
mwanzo sura 3:15 “nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke,kati ya uzao wako
na uzao wake;yeye atakiponda kichwa chako nawe utamwuma kisigino chake.”,Luka
1:28-“malaika akamwendea,akamwambia,’salamu,ewe uliyeneemeshwa na Mungu!Bwana
yuko nawe!”, na Luka 1:41 –“mara tu Elizabeth aliposikia sauti ya maria,mtoto
mchanga tumboni mwake Elizabeth akaruka. Naye Elizabeth akajazwa Roho
Mtakatifu. Mwanzo 3;15 inatafsiriwa kama uzao wa Eva (ie kristo Yesu)
atamshinda Yule mwovu,lakini Yule mwovu pia atawatesa wafuasi wake kwa
kuwashawishi kutenda dhambi
Hali hii
mpendwa msikilizaji iliwapelekea wababa wakanisa kumwona mwanamke
anayezungunziwa katika mwanzo 3;15 kama kivuli cha Bikira Maria mama wake
Kristo. Wataalamu wengi wakisasa wa teolojia
wanasema kutokana na mwanga wa aya hii kuwa ushindi wa mama huyu dhidi
ya Yule mwovu usingewezekana kama alikuwa na dhambi. Hivyo mama huyu aliingia
duniani bila dhambi ya asili
Tafakari nzuri, asante sana
ReplyDelete