Home » » MARIA ANAZUNGUMZA NA WANAWE

MARIA ANAZUNGUMZA NA WANAWE



MARIA ANAZUNGUMZA NAWEWE
MATANDA RICHARD TESHA
Kila kitu ninachokushirikisha mwanangu mpendwa, si chako peke yako bali ni kwa wanangu wote ninaowapenda kupita kila kitu. Ujumbe huu ni kwa wote wanaompenda mama yetu mpendwa Bikira Maria. Ubaki daima katika  moyo wangu na kuwa mwaminifu kwangu mwanangu.
1.      Nitakuwa  daima nawe.
Weka maazimio yako kwa moyo wangu safi, wewe ni wangu na mali yangu.  Kila  muda au wakati uwe kama ninavyopenda,fanya ninavyopenda. Usiogope kwani nitakuwa karibu nawe. Niko kwenye harakati za kukuandalia mambo makuu zaidi lakini kidogo kidogo kama mama anavyo mfanyia mwanae.

2.      Utume wako
Leo ninafuraha kubwa sana nawe kwani umekaa karibu sana na moyo wangu. Unaona vitu vya ulimwengu  huu jinsi vilivyo mbali nawe na visivyo vya kueleweka mbele yako. Unatazama na kuona vitu hivyo vinavyokuchosha ambavyo si mimi mama yako ninayekupenda  kama ulivyo.
Jifunze kupagawa nami ili kila kitu ufanyacho,  nitakuwa ni mimi ninayefanya kukupitia wewe. Na ninapenda kutenda kukupitia wewe. Utateseka sana lakini jipe moyo kwani daima nitakuwa nawe.

3.      Sababu ya machozi yangu
Nimefarijika sana asubuhi ya leo. Ulipokuwa unatazama sanamu yangu inatoa machozi na pia umekuja misa ili kuufariji moyo wangu safi. Nimefurahia mawazo yako ya uwana na upendo. Ni kweli nimefarijika
Machozi yangu ni kwa sababu ya watoto wangu wasio mjali Mungu tena na kujizamisha katika furaha za ulimwengu huu. Nalia pia kwa ajili ya wanangu mapadre ambao hawanijali tena, wanakufuru na kumwacha mwanangu peke yake kwenye tabernakulo. Kila mmoja nampenda kivyake . nakuomba uwaombee hawa mapadre kwani wao wamekabidhiwa dhamana kubwa ya kuwaokoeni.

4.      Nitakuwa kiongozi  wako
Natambua kabisa unajiona kuwa hufai kwa utume wangu na kuniuliza kwanini                  “ hukuchagua mtu mwingine anayefaa na mwenye uwezo?” na kwa nini unanitegemea  na unajua madhaifu yangu yaliyopita?
Mwanangu nimekuchagua kwa sababu ya udhaifu wako na hakuna mtu atakayesema kuwa hii ni kazi yako. Nitadhihirisha uwezo  wangu kutokana na udhaifu wako. Kwa utupu wako kiakili nitadhihirisha uwezo wangu. Mimi mwenyewe nitakuwa kiongozi wa jeshi langu. Kusiwepo na kiongozi mwenu mimi nitaongoza yote.
Kitu cha pekee ninachotaka kutoka kwako ni kukubali uongozi wangu kwa moyo wako wote kama vile mwanangu alivyojitoa kabisa kwangu na kuniamini ndipo nitakuwa mlinzi wa kila kitu katika maisha yako.

5.      Acha mimi niwe mtendaji.
Kwanini unahangaika na kuwa na wasiwasi? Tambua unaongozwa na mimi. Kujitolea kabisa kwangu kuna maanisha kujiachia kabisa kwangu nikuongoze kama vile mtoto alivyo kwa mama yake.

6.      Mimi daima ni mama.
Je! Unapendezwa na nyumba ninayokutengenezea? Hujawahi kuota kuwa itakuwa hivyo kwenye pango katika miamba.. najua hukuwa na habari  kwamba nilikuwa nakuandalia nyumba hiyo. Ulipokuwa unatenda kwa ajili yangu, ukiteseka kwa joto na uchovu, ungeweza kusema ‘ni furaha iliyoje kufanya kwa ajili ya mama yangu mpendwa Maria. Nilikuwa nakufikiria na kukuandali mahali pa kupumzika. Nimekuleta mahali hapa nikijua ni pazuri kwako na kwangu. Kuna mwingine anaye nipenda sana. Kuna watoto wengine wengi wanaonipenda. Wewe ni mojawapo wa hao wanaonipenda.

7.      Uwe mwangalifu na mwenye kusali
Wako mapadre ambao wameacha ujumbe wa injili na kung’ang’ania malimwengu na kujikita zaidi katika utajiri. Ni kwa sasbabu hii ulimwengu utaangamia kwa sababu yao. Ni wanangu nyie mnaonipenda ambao mtakaoleta mageuzi katika ulimwengu huu. Nami nitakuwa pamoja nawe katika dhoruba zinazokusonga.

8.      Mioyo ya mapadre wangu
Uwe nami moyonni kila mara utapata amani. Usihofu kwa ajili ya lipi utakalofanya. Yule ambaye amejitolea kwangu , ni wa kwangu kabisa na hawezi kabisa kuchagua yeye binafsi anachotaka kufanya. Ukibaki ndani mwangu nitakwambia kipi cha kufanya kwa wakati husika.
Nimekupokonya mikononi mwa maadui wangu sasa umechukua njia kuelekea fadhila ya upendo, ili chochote kifanyike kadri ya matakwa yangu. Nitakushika mkono na tutafanya yote pamoja. Nakuonea wivu  kwa kuwa name mama yako mpendwa.
Wambia kwamba nataka kitu kimoja kutoka kwao yaani kujitoa kabisa kama watoto wangu,wakiachilia yote kwangu kiwe kizuri au chenye heshima na kunipa mioyo yao. Ndipo nitakapokuwa mama yao sawa sawa.: msomaji unaweza kutoa maoni yako kwa ajili ya kuboresha

0 comments:

Post a Comment

RICHARD MATANDA TESHA

 
Support : Richie | Bikira Maria | Elimu Endelevu
Copyright © 2013. BIKIRA MARIA - All Rights Reserved
Template Created by Mwariko Published by Mwariko team
Proudly powered by Jicho la Habari