Home » » BIKIRA MARIA NI NANI

BIKIRA MARIA NI NANI


NI MAMA WA MUNGU, NI MAMA ALLIYEKINGIWA DHAMBI YA ASILI, NI BIKIRA DAIMA NA NI YULE ALIYEPALIZWA MBINGUNI MWILI NA ROHO. Waswahili  wanamsemo wao wasemao  kuwa Mti wenye matunda ndio upigwao mawe. Mpendwa katika Kristu ukiwa mtu mwema daima tarajia kupata makombora kutoka kwa majirani zako kwasababu ya wema wako. Ukiona huna makombora yoyote kutoka kwa wenzako tambua unakasoro Fulani. Maria mama yetu amekuwa akipata makombora  au  mashambulizi kutoka kila upande kuanzi kipindi kile cha kanisa la awali  ambapo mzushi mmoja Nestory alikataa kabisa Bikira Maria kuitwa mama wa mungu.  lakini hii kwa mtu anayefahamu msemo huo ataacha kabisa  kumsema mama vibaya.
inawezekana  kuwa Maria mama yetu anayetupenda akawa tena chanzo cha kujenga ukuta kati ya wakatoliki na waprotestant? Swali hili nitalijibu tunavyoendelea.
Mwaka  juzi mtu mmoja alitembelea nchi mbalimbali duniani zikiwemo Kenya,Kongo, na Rwanda. Kila mahala alipokwenda aliulizwa swali ni kwa namna gani watajibu waprotestant maswali wanayowatupia kuhusu Bikira Maria.
 Inaonekana  leo hii katika vitabu mbalimbali vinavyo chapishwa kumhusu Maria kwamba makanisa makubwa ya kiprotestant taratibu yameanza kumtambua binti huyu wa Nazareth. Hii inatokana na tafakari yao juu ya maneno yote aliyosema mwanzilishi wao Martin Luther. Ambaye katika uhai wake alisema “maria ni kweli mama wa Mungu” na akawa anaimba nyimbo mbalimbali zikiwemo za kumsifu mama kama vile SALVE REGINA wimbo ulioimbwa hapo zamani na mwishoni mwa wimbo huu maneno “ BIKIRA MARIA yalisikika. Ndugu zangu wimbo huu hata leo hii bado unasikika katika baadhi ya makanisa.
Sasa tuangalie picha ya mama yetu ndani ya Biblia ambayo inawakilisha wakristo wote. Mama huyu alimpenda Kristo mpaka akawa mfuasi wake  na sasa kwa namna ya pekee yuko katika roho ya kila Mkristo kama mwombezi wake. Wewe unayenisikiliza tambua kuwa mama yuko tayari kukuombea anza sasa kama ulikuwa bado.
Ni kweli kwamba waprotestant wanauliza wakatoliki maswahili mengi  kwa kile wanachosema na kusikia kuhusu ibada kwa Bikira Maria  wanazofanya. Na wakatoliki kwa upande wao nao huwauliza maswali waprotestant kuhusu unyamavu wao juu ya sifa kemkem ambazo zinamhusu mama zilizoandikwa ndani ya Injili.
Sisi  tunaomfahamu mama yetu tunaalikwa leo kujua kuwa jina protestant ni mkusanyo wa makanisa mengi. Mfano waorthodox ambao si wakatoliki lakini wanaonesha upendo wa pekee kwa mama ambao unafanana kwa karibu sana na wa kikatoliki.
Waothodoxy wanaenda mbali zaidi kuliko wakatoliki kwa namna wanavyo mheshimu B.M katika tenzi zao na kwenye sikukuu zao mbalimbali zinazomhusu mama. Vipo viashiria vingi katika makanisa yao vinavyoashiria jinsi mama alivyo mama wa Mungu ( theotokos).
Maria alimpenda mwanae na akajitoa kabisa kwake. Kama  vile haikutosha anatupenda nasi pia kwa kuwa Kristo alitufikia kumpitia mama Maria. Kama mama atafahamika vizuri na kazi zake atakuwa kwetu chanzo cha umoja ingawa tuna utofauti wetu wa kikabila,kidini,kitaifa na kimazingira.
sasa  tuangalie jinsi mama alivyokuwa mfuasi kamili wa mwanae. Mama alikuwa wa kwanza kuinjilishwa habari njema na malaika Gabriel na alikuwa wa kwanza kumfanya Kristo awe kitovu cha maisha yake. Nakualika umfanye sehemu ya maisha yako nawe utabarikiwa sana.
Mpendwa mama maria ndiye aliyekuwa wa kwanza kusema ndiyo kwa Mungu,kule kukubali kuwa mama wa mungu. Na ndiyo yake hii inakuwa mwanzo wa ndiyo zote wanadamu wanazoonesha kwa Mungu wao katika yote watendayo. Ndiyo ya mama , ilitangulia ndiyo ya mtakatifu Yosefu aliyekubali kumchukua na kumwacha kwa siri baada ya kuambiwa na malaika kwamba anaujauzito kwa uwezo wa roho mtakatifu. Ndiyo yake inarithiwa kutoka kizazi hadi kizazi,karne hadi karne na kutufanya tutoe ndiyo zetu mbele ya Mungu.
Kumpitia mama, Kristo alipendwa mpaka watu walidhiriki kusema “heri maziwa aliyonyonya” jamani! Kumbe hata maziwa ya mama yalibarikiwa! Sembuse utu wake mzima? Mama alibarikiwa sana amini hilo.
Mpendwa mama yetu alikuwa mmisionari wa kwanza. Alifunga safari kutoka Nazareth mpaka AIN KARI akimbeba Yesu akipitia barabara zilizochongwa na wanadamu mpaka kwenye familia ya mbatizaji. Na kupitia Elizabeth, mama yake Yohani mbatizaji,familia hii ilikiri bila kusita imani ya Kikristu kwa kusema – mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu aje kwangu?. Mpendwa kila Mkristo wa kweli anatambua kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Mpendwa kwa kuwa karibu na mama, nawe utakuwa mzazi wa Yesu na daima utambeba daima katika moyo wako na daima utachagua mema kama mama alivyofanya.
Mmisionari wa jana, leo na kesho wote wanafuata nyayo za mama kwa kumbeba Kristo na kumpeleka kwa wahitaji.
Je! unaelewa mtu wakwanza kubarikiwa katika Injili , ni mama yetu Bikira Maria na akawa wakwanza kutangazwa mwenye furaha kwa sababu ya imani yake . hivi nikuulize umeshawahi kufurahi kwasababu ya imani yako? Kama sivyo  ni kwa nini? Jifunze leo kutoka kwa mama aliyetanganzwa kuwa mtu wa kwanza kusifiwa kwasababu ya imani yake.

1 comments:

  1. endelea kusoma mafunzo haya kwa upanuzi zaidi wa uelewa wako. kuhusu mafunzo sahihi ya Kanisa kujhusu mama yetu Bikira Maria.

    ReplyDelete

RICHARD MATANDA TESHA

 
Support : Richie | Bikira Maria | Elimu Endelevu
Copyright © 2013. BIKIRA MARIA - All Rights Reserved
Template Created by Mwariko Published by Mwariko team
Proudly powered by Jicho la Habari