Huyu ndiye Padre RICHARD MATANDA TESHA wa Jimbo katoliki Moshi. Alizaliwa
Tarehe ya 26/06/1972.na ni mzaliwa wa Parokia Ya Uru– Shimbwe.
Baada ya masomo yake ya Msingi alijiunga na seminari ya Mt.Yakobo “St. James
seminary” mwaka 1991– 1996
Na hatimaye masomo ya falsafa (Philisophy) katika chuo cha Kibosho– Moshi
kwa miaka mitatu. Na hatimaye Masomo ya teolojia ( huko Segerea Dar-Es-Salam.)
Na kwa miaka niwili chuoni Mwanza SAUT akisomea
mawasilianoya jamii na masoko. Tuzidi kumwombea kwa changamoto mbalimbali
anazokumbana nazo katika utume wake ili azidi kumhubiri Kristo msulubiwa.
Mwandishi huyu amekuwa akijituma katika kuandika vijitabu mbalimbali kuhusu
mama yetu mpendwa Bikira Maria na kutoa tafakari mbali mbali
katika taasisi na kwenye vyombo vya habari hasa Redio Maria. na Redio SAUT ya
Jijini Mwanza.
ameandika vitabu mbalimbali kama:TAFAKARI NA PADRE
MATANDA, cha pili JE! UNAMJUA HUYU na cha tatu MSAMAHA
ISHARA YA UPENDO ambacho amekiandika akiwa Huruma Hosptal Januari hadi
Febrari 2014 .
Padre Richard Matanda Tesha anatumia mang’amuzi aliyoyapata shuleni katika
Masomo yake ya Philosophy na Theology na tafakari zake binafsi ili kuelimisha jamii. kwa sasa anapatikana Mango Parish kuanzia 12/03/2014
0 comments:
Post a Comment